MBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John
Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM
kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 2104
sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata kura 253 sawa na 10.5% na
Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda
ndiye aliyepewa jukumu la kusoma mshindi katika kura za Kikao cha
Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi
mkoani Dodoma.
KURA ZILIZOPIGWA: 2422
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416
SHARE HII HABARI NA RAFIKI ZAKO:
Related Posts:
0 comments:
Post a Comment