Clement Mwankayi Kiondo ‘CK’ akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Wawili hao walipandishwa kizimbani juzi (Alhamisi) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Katika kosa la kwanza, CK alidaiwa kutenda kosa la kughushi hundi no
302002 yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 100 kutoka kwenye Ofisi ya
Waziri Mkuu huku akijua kuwa ni kosa kisheria.
Katika kosa la pili, CK ambaye aliwahi
kudaiwa kumgombanisha Wema na Kajala Masanja kwa pamoja na Emmanuel,
mnamo Machi 13, 2014 walikula njama za kuiba kiasi cha Sh. milioni 100
katika Benki ya NBC, Tawi la Ilala jijini Dar.
Kesi
hiyo ambayo ilisikilizwa mbele ya Hakimu Huruma Shahid na Wakili wa
Serikali, Aloyce Mbumito, ilidaiwa mnamo Machi, 2014 kwa nyakati
tofauti, jamaa hao walitumiwa kughushi hundi kwenye ofisi hiyo ya Waziri
Mkuu.
Katika kesi hiyo watuhumiwa hao
walipaswa kuwa na wadhamini wawili-wawili wanaotambulika na kiasi cha
Sh. milioni 10 kila mmoja kwa ajili ya kupatiwa dhamana.


0 comments:
Post a Comment